Programu Zitakazo Muwezesha Mwanafunzi Kusoma Akiwa Nyumbani.

Ugonjwa wa Corona  unaendelea kutesa Dunia huku viongozi, wanasayansi na watalaamu   wa afya wakiendelea kutafuta chanjo na dawa ya ugonjwa huo unaosambaa kwa kasi duniani.

Sekta ya elimu ni  kati ya sekta iliyo athirika sana kutokana na ugonjwa huu. Serikali imefunga shule zote za awali, msingi, sekondari na vyuo ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu  hatari. Wanafunzi wote wametakiwa kubaki nyumbani ili kuwakinga na maambukizi wakati serikali ikifanya jitihada za kupambana na ugonjwa huu. Hii ni katika  hatua ya   kuwalinda wanafunzi na waalimu dhidi ya maambukizi. 

Kila mzazi, ana jukumu la kuhakikisha mwanae ana jisomea awapo nyumbani mpaka pale shule zitakapo funguliwa. Je unafahamu programu za simu janja zinazo tumia android zitakazo muwezesha mwanao kujisomea akiwa nyumbani? Hizi ni baadhi ya programu ambazo mzazi anaweza kuwanazo kwenye simu zitakazo mwezesha mwanafunzi kujisomea katika kipindi hiki cha likizo ya dharula .Bonyeza maandishi ya blue ili kuweza kupakuwa (download) programu hizi moja kwa moja kwenye simu yako.

Ubongo Kids

Hii inawahusu zaidi watoto ambao wanajifunza kusoma na kuhesabu. Kampuni ya Ubongo wana programu mbalimbali zitakazomwezesha mtoto kujifunza kwa wepesi kama vile hesabu za panya, treni ya namba na herufi na akili. Programu zao zipo katika lugha ya kiswahili na kingereza.

Shule Direct

Hii hutoa maudhui mbalimbali kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kama vile notes majaribio na mitihani ya kujipima. Vyote hivi vinapatikana kupitia programu hii lakini pia unaweza kuvipata kwa kutembelea tovuti yao.

 

Mtabe App

Mtabe ni programu inayokupa majibu ya maswali yako ya shule kwa wanafunzi wa sekondari. Mwanafunzi anaweza kuuliza maswali mbalimbali ya masomo na akapata majibu. Programu hii inawasaidia wanafunzi kukuza uelewa wao na kupanua maarifa.

 

Khan Academy

Hii ni programu nzuri sana kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Programu hii ina video a masomo yote kuanzia fizikia, kemia, jeografia, historia . Pia ina maswali yatakayo wawezesha wanafunzi kujipima uelewa na mwanafunzi anaweza kupakua video na kuzihifadhi kwenye simu na ataweza kuzitazama pale ambapo hana mtandao.

 

Khan Academy Kids hii app ni nzuri kwa watoto hutumia michezo (games) mbalimbali katika kufundishia kuumba herufi na kuhesabu maumbo mbalimbali. Programu hii ina video mbali mbali za masomo kwa wanafunzi kuanzia chekechea mpaka darasa la saba. Programu hii inatumia lugha ya kiingereza hivyo inawafaa zaidi wanafunzi wa shule za msingi zenye kutumia mtaala wa kingereza.

Sema Run

Programu hii ni nzuri kwa watoto kujifunza kusoma na kuandika lugha ya kingereza. Imetengenezwa katika namna ya kuwafurahisha na kuwachangamsha watoto huku ikiwafundisha alfabeti za kingereza na kuwapa mazoezi mbalimbali ya kusoma na kuandika.

Hapa nchini, Serikali pamoja na wadau wengine wameandaa programm mbalimbali zinazoendelea kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa nyumbani. Programu hizi za vipindi vya video na redio na majukwaa ya mtandaoni kwa wanafunzi wa vyuo ni nyenzo muhimu kuhakikisha wanafunzi wanatumia muda wao vizuri.

Wazazi wana jukumu la kuhakikisha wanafunzi wana nufaika kutokana na jitahada hizi ili kuwasaidia wanafunzi kujiendeleza kimasomo wakiwa nyumbani.

Camara Education Tanzania tutaendelea kukuletea makala mbalimbali zitakazo kuelimisha na kukushauri namna bora za kumsaidia mtoto wako katika kipindi hiki. Endelea kufuatilia mfululizo wa makala zetu kila wiki kupitia tovuti yetu na mitandao ya kijamii. Kwa maoni au ushauri usisite kuwasiliana nasi.

 

Comments are closed.