Dondoo za Kumuandaa Mwanafunzi kabla ya kurejea shuleni.

Siku za hivi karibuni nchi nyingi zimeanza kufungua shule katika kuendelea kupunguza taharuki dhidi ya ugonjwa  wa CORONA. Nchi nyingi zimekua zikilegeza masharti ya watu kubaki majumbani na kuwataka kuendelea na maisha huku wakizingatia tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa wa afya.

Kufunguliwa kwa vyuo na kidato cha sita katika nchi yetu ni ishara kuwa huenda madarasa yalio salia  yakarejea shuleni kama hali itaendelea kuwa nzuri kama ilivyo hivi sasa. Kama mzazi, una wajibu wa kumuandaa mwanao ili aweze kurudi shuleni baada ya kukaa nyumbani kwa kipindi kirefu, Walimu na wadau wengine wana nafasi kubwa ya kuwasaidia wazazi katika jukumu hili. Yafutayo ni baadhi ya mambo ya kufanya ili kumuandaa mwanao aweze kurejea shuleni katika namna bora.

Kumtoa hofu na kumuhakikishia usalama

Mzazi unapaswa kumtoa hofu juu ya muenendo wa ugonjwa wa Corona na kumtia moyo kuwa ni wakati sahihi wa kurejea shuleni. Fanya maongezi na mwanao huku ukinukuu vyanzo sahihi vilivyo toa taarifa juu maendeleo ya ugonjwa wa Corona nchini na kuruhusu masomo kuendelea. Kurudi shule akiwa ni hofu kunaweza kupelekea kushindwa kufanya vizuri katika masomo yake.

Mzazi Akizungumza na mtoto wake.

Elimu juu ya kuendelea kujikinga na ugonjwa wa Corona

Kama viongozi mbalimbali wa serikali walivyosema, Corona imepungua sana lakini haijanisha. Hivyo, kufunguliwa shule haina maana kua ugonjwa wa Corona ni umeisha. Lengo la serekali ni katika kuhakikisha maisha yanaendelea na gonjwa hili halikwamishi shughuli za msingi za kujenga Taifa. Ni muhimu mzazi kumkumbusha mwanafunzi namna bora ya kujikinga na umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari awapo shuleni kwani ni sehemu inayobeba watu  wengi wanaotoka sehemu mbalimbali.

Muandae Kimasomo

Mtoto Akijisomea.

Mzazi hakikisha katika kipindi hiki kilicho baki mwanao anajisomea hasa yale aliyofundishwa wiki chache kabla ya shule kufungwa. Kuna jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali kama vile vipindi vinavyoendelea kurushwa redioni na kwenye televishioni na majukwaa mbalimbali ya mitandao, Hizi zote ni fursa kwa mwanao kujisomea na kujiandaa kabla shule hazijafunguliwa.

Anza kumzoesha mazingira ya shule

Pindi shule zitakapo tangazwa kufunguliwa ni vizuri kumsaidia mwanao kwa kuanza kumzoesha mazingira ya shule, Unawea kumpigia simu mwalimu wake na kumpa aonge nae, kumkutanisha na rafiki zake wa shule ili waweze kujiandaa au kujadiliana au kutembelea shule yake siku chache kabla masomo hayajaanza. Hili litamfanya aweze kujiandaa kisaikolojia kabla ya masomo kuanza.

Baadhi ya vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona

Muandalie mahitaji yote muhimu

Kama ilivyo ada, shule zinaoi funguliwa kuna mahitaji mbalimbali mzazi/mlezi anapaswa kuandaa kama sare za shule, daftari, kalamu, vitabu nk. Kutokana na janga hili la Corona, mahitaji mapya yameibuka kama sabuni, vitakasa mikono na barakoa. Ni muhimu kuandaa mahitaji haya mapema ili upate muda wa kutosha kuhakikisha mwanafunzi amepata mahitaji yote ya muhimu.

Mpe Ari na sababu za kwenda kufanya vizuri shuleni

Kwakuwa wanafunzi engi wamekaa nyumbani muda mrefu tofauti na miaka mingine, huenda ari ya kujisomea ikawa imepungua. Wazazi waendelee kuwakumbusha watoto umuhimu wa elimu kumsisitiza mwanafunzi akafanye vizuri katika masomo yake. Msaidie mwanafunzi ajiwekee malengo ya kufanya vizuri na mpe sababu ya kufanya hivyo.  Hii itawajenga kisaikolojia pindi watakaporudi shuleni na kuona ni mazingira ya kawaida kwao.

Kama ilivyo ada, shule zinafunguliwa kuna mahitaji mbalimbali mzazi/mlezi anapaswa kuandaa kama sare za shule, daftari, kalamu, vitabu nk. Kutokana na janga hili la Corona, mahitaji mapya yameongezeka kama vitakasa mikono na barakoa. Ni muhimu kuandaa mahitaji haya mapema ili kuhakikisha mwanafunzi amepata mahitaji yote ya muhimu.

KUMBUKA! Elimu ni bahari, haina mwisho. Ni jukumu la mwanafunzi, mzazi, mlezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto wanapata elimu katika mazingira salama na wezeshi kwao. Wazazi, walezi, walimu, serekali na asasi za kiraia kwa ujumla hili ni jukumu letu. Kwa pamoja, tushirikiane kuhakikisha upatakanaji wa elimu bora katika ngazi zote

Comments are closed.